31 Mei 2024 - 14:29
Katibu Mkuu wa UN ashiriki kikao cha kumunezi hayati Raisi katika Baraza Kuu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amepongeza ufahamu wa kisiasa wa hayati Ebrahim Raisi wakati wa kikao kilichofanyika katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kumuenzi rais huyo wa Iran aliyekufa shahidi katika ajali ya helikopta akiwa a wenzake kadhaa.

Baraza hilo liliandaa kikao hicho maalumu Alhamisi, chini ya wiki mbili baada ya ajali hiyo.

Guterres alisema,  Rais Raisi aliiongoza Iran katika wakati mgumu kwa nchi, kanda na kimataifa na kubainisha kuwa: "Saa chache kabla ya kifo chake, Rais Raisi alikutana na mwenzake wa Jamhuri ya Azerbaijan kuzindua bwawa la Qiz Qalasi, mradi mkubwa zaidi wa pamoja kati ya nchi hizo mbili."

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alisema: "Katika nyakati hizi ngumu, ushirikiano wa kimataifa na wa kikanda kwa kweli unahitajika zaidi kuliko hapo awali" na kuongeza kuwa, "ushirikiano huo ni muhimu ili kujenga imani, kuzuia migogoro, na kutatua migogoro."

Raeisi na msafara wake, akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian, walikufa shahidi shahidi baada ya helikopta iliyokuwa imewabeba kuanguka ilipokuwa njiani kuelekea Tabriz, mji mkuu wa Mkoa wa Azarbaijan Mashariki mwa Iran.Mkasa huo ulifuatiwa na mijumuiko ya mazishi ya mamilioni ya watu huko Tabriz pamoja na mji wa kaskazini-kati wa Qom na mji mkuu Tehran na kisha mji wa Mashhad.

Guterres kwa mara nyingine tena ametuma salamu za rambirambi kwa familia za marehemu pamoja na serikali na taifa la Iran.

Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa  Amir Saeid Iravani kufanyika kikao hicho za kumuenzi Shahidi Raisi katika Umoja wa Mataifa ni ishara ya heshima ya dunia kwa taifa la Iran na mashahidi wa ajali ya helikopta.


342/